Mwanamke mpalestina auawa na Waisraeli

Image caption Mwanamke mpalestina auawa na Waisraeli

Polisi wa Israili wanasema kuwa Mpalestina amepigwa risasi na kuuawa, baada ya kuvurumisha gari lake kulenga kundi la Waisraili, na kuwajeruhi wanne.

Shambulio hilo limetokea katika ufukwe wa Magharibi unaokaliwa.

Punde baadaye, mwanamke wa Palestina alipigwa risasi na kujeruhiwa, kama inavoripotiwa, alipojaribu kumdunga kisu mlinzi, karibu na eneo la walowezi wa Ki Yahudi.

Hayo ndio matukio ya karibuni kabisa, katika wimbi la ghasia za majuma ya karibuni, ambayo yamesababisha vifo vya Waisraili 11, na zaidi ya Wapalestina 70.