Ugonjwa wa Malale wadhibitiwa, Uganda

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Mbung'o wanaoambukiza ugonjwa wa Malale

Maelfu ya watu nchini Uganda wameokolewa maisha, kutokana na mradi wa kusaidia kuutokomeza ugonjwa wa Malale

Watafiti kutoka Scotland wamesema bila ya kupata matibabu, ugonjwa huo unaoambukizwa na mbung'o ni janga.

Katika jitihada za kuhakikisha maambukizo ya ugonjwa huo hayasambai kwa binadamu nusu ya milioni ya ng'ombe walioko maeneo ya vijijini nchini Uganda wamechomwa sindano ya kuua vimelea vya ugonjwa huo. Matokeo yake ni kupungua kwa asilimia 90 ya wagonjwa.

Wanasayansi kutoka katika Chuo Kikuu cha Adinburgh wana matumaini kuwa mradi huo, utasambaa pia katika maeneo mengine ya Uganda.

Shirika la Afya la Umoja wa mataifa linaamini kuwa huwa kuna wagonjwa takriban 30,000 wa ugonjwa huo wa Malale kila mwaka barani Afrika.