Viongozi wa Afrika kuzungumzia usalama

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Utapakaaji wa silaha ovyo kunatishia amani ya Afrika

Mkutano wa awamu ya pili wa amani na usalama barani Afrika utafanyika mjini Dakar nchini Senegal.

Kwa siku mbili, viongozi wa nchi, mawaziri na wataalamu wa jeshi wataangalia njia bora za kuimarisha usalama na utulivu barani Afrika.

Mkutano huu unafanya wakati ambapo nchi kadhaa barani Afrika zimeshuhudia machafuko mwaka huu.

Mkutano huu wa kimataifa wa awamu ya pili unalenga zaidi changamoto za bara la Afrika na athari zake katika ngazi za kimataifa. viongozi wanatarajia kujadiliana namna ya kupata suluhu ya kuimarisha amani na usalama wa bara la Afrika.

Mada hizi mbili ni muhimu na zinawakilisha pingamizi katika usalama wa kimataifa na ukuaji wa uchumi kwa mujibu wa Rais wa taasisi ya Pan Afrika iliyopo mjini Dakar, cheikh Tidiane Gadio.

Mkutano huo unalenga katika kupanua wigo na mawasiliano ya moja kwa moja kwa kuimarisha mikakati ya kiafrika na ushirika wa kimataifa kwa lengo la kuwawezesha Waafrika kuwa na mipango yao wenyewe. Warsha mbalimbali zitaelekezwa katika masuala kadhaa ikiwemo kupiga vita masuala ya itikadi kali, uharamu na uhamiaji haramu.

Mkutano huu, utajumuisha zaidi ya wajumbe mia tano wakiwemo wanazuoni wataalamu waliobeba katika masuala mbali mbali na wajumbe kutoka taasisi za kiraia.

mkutano huu unatakiwa ukimalizika basi uwe na mkakati wa pamoja wa jinsi ya kukabiliana na changamoto ya usalama ambayo inaathiri bara zima.