Mexico kujadili kuhalalisha bangi au la

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mexico kujadili kuhalisha bangi au la

Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto, anasema kuwa ataanzisha mjadala wa taifa kujadili iwapo wanainchi wanataka baingi iidhinishwe au la.

Tangazo lake linakuja juma moja tu baada ya Mahakama ya nchi hiyo kuwapa idhini watu wanne tu kukuza bangi kwa matumizi yao ya kibinafsi.

Rais anasema kuwa watalaamu sasa wanafaa kuja pamoja ili kujadili hatma ya baadaye ya uidhinishwaji wa bangi nchini Mexico.

'Nahisi kama madaktari,wasomi na pia wanasoshiolojia wanapaswa kutoa mchangao wao katika mjadala huu'' alisema Bwana Nieto.

''Mimi mwenyewe napinga kwa kinywa kipana uhalalishwaji wa bangi '' aliongezea rais Pena Nieto, hata hivyo '' maoni yangu ya kibinafsi hayatazuia kufanyika kwa mjadala huo wa taifa''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mahakama ya nchi hiyo kuwapa idhini watu wanne tu kukuza bangi kwa matumizi yao ya kibinafsi.

Mexico ni moja wa mataifa yaliyoathirika vibaya na ghasia zinazotokana na magenge ya walanguzi wa madawa ya kulevya.

Vilevile baadhi ya wadau wanashauri kuwa kuhalalishwa kwa bangi na mihadarati Mexico na Marekani kutawaondoa walanguzi wa madawa ya kulevya kwenye biashara hiyo na hivyo kupunguza idadi ya watu wanaouawa katika vita dhidi ya ulanguzi.