Senegal yatangaza vita dhidi ya wapiganaji

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Macky Sall wa Senegal

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza vita dhidi ya mfumo wa uanzishwaji wa makundi ya wapiganaji wa kijihadi.

Amesema kuwa viongozi wa kiislamu wanapaswa kuelimishwa ili kukuza 'uislamu wa uvumilivu'.

Bwana Sall,ambaye ni muislamu pia ametaka kuwepo kwa ushirikiano wa kiintelijensia miongoni mwa serikali.

Wiki iliopita,maafisa wa Senegal walisema kuwa maimamu wawili walishtakiwa kwa kushiriki katika fedha chafu mbali na madai ya ushirikiano wa makundi ya wapiganaji.

Mataifa mengine ya Afrika Magharibi ikiwemo Nigeria na Mali yanapigana dhidi ya wapiganaji wanaoshirikiana na kundi la kigaidi la al-Qaeda au lile la islamic state.