Rais wa Myanmar ampongeza Suu Kyi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bi Aung San Suu Kyi

Rais wa Myanmar Thein Sein amekipongeza chama cha upinzani cha Aung San Suu Kyi kwa kushinda uchaguzi mkuu, msemaji wake ameiambia BBC.

Huku ikiwa asilimia 47 ya viti vimetangazwa, Chama cha Nationa League for Demokrasi kimechukua asilimia 90 ya kura.

Bi Suu Kyi ameuandiakia uongozi akitaka mazungumzo ya uwiano wa kitaifa.

Lakini msemaji U Ye Htut amesema mkutano kama huo unaweza kufanyika tu baada ya matokeo rasmi kutangazwa.

Amesisitiza kuwa hakuna jaribio lolote la kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo hayo ya uchaguzi wa siku ya jumapili.

Image caption Rais wa Myanmar Thein Sein

Waandishi wanasema bi Suu Kyi anafuatilia mambo kwa tahadhari licha ya ushindi wake mkubwa.

Chama cha NLD kilishinda uchaguzi wa mwaka 1990,kabla ya matokeo hayo kufutiliwa mbali huku bi Suu Kyi akiwekwa katika kifungo cha nyumbani cha mda mrefu.

Chama tawala cha kijeshi Union Solidarity Development Party {USDP} kilichoshinda uchaguzi uliopita ambao ulikosolewa miaka mitano iliopita kufikia sasa kina asilimia 5 ya viti vionavyogombewa nchini humo .

Robo ya viti vya ubunge huwekewa wanajeshi.