Ugonjwa wa Uti wa mgongo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kinga dhidi ya uti wa mgongo

Wataalamu wa afya wanasema mpango wa chanjo kwa umma dhidi ya homa ya uti wa mgongo barani Afrika umepata mafanikio makubwa.

Zaidi ya watu milioni mbili walipata kinga dhidi ya maradhi hayo katika nchi zipatazo 16 barani Afrika, kutoka Gambia mpaka Ethiopia.

Shirika la Afya Duniani limesema katika kipindi cha mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa wanne tu, katika bara hilo ambalo awali liliweka rekodi ya kuwa na maelfu ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo, kila mwaka.

Kampeni ya kupambana na ugonjwa huo ilianza mwaka 2010.