Hazina ya $1.9bn kwa Afrika yaidhinishwa

EU Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mamia ya watu wamekuwa wakifariki baharini wakijaribu kufika Ulaya

Viongozi wa Muungano wa Ulaya na Afrika wametia saini makubaliano yanayotarajiwa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaofunga safari hatari ya kutaka kufika Ulaya.

Viongozi hao wa EU, kwenye mkutano Malta, wameidhinisha kuundwa kwa hazina ya $1.9 bilioni za kusaidia mataifa ya Afrika.

Baadaye, viongozi hao watafanya mkutano usio rasmi ambapo watajadili suala ya uhamiaji Ulaya, yakiwemo mataifa ya Balkan.

Muungano wa Ulaya unakadiria kwamba watu 3 milioni huenda wakafika Ulaya wakitafuta hifadhi au nafasi za kazi kufikia 2017.

Miongoni mwa mataifa yatakayofaidi kutokana na hazina hiyo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Djibouti, Somalia, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia.