Wakurdi wajaribu kukomboa mji kutoka kwa IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mji wa Sinjar ulitekwa na wapiganaji wa IS mwaka jana

Wapiganaji wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq wameanzisha operesheni ya kuukomboa mji wa Sinjar, ulioko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Syrian kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State.

Operesheni hiyo inasaidiwa na muungano unaoongozwa na Marekani kupitia mashambulio ya ndege kutoka angani.

Kuuokomboa mji wa Sinjar kutaziba mawasiliano kati ya ngome mbili za IS Raqqa na Mosul.

Mji huo ulipotekwa na IS mwaka jana, mamia ya maelfu ya watu wa dini ya Yazidi walikwamba baada ya kutorokea mji wa Sinjar.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yazidi wakitoroka mlima Sinjar mapema mwaka huu

Mamia ya wanaume waliuawa na wanawake wa Yazidi wakatekwa na kutumiwa kama watumwa wa ngono.

Shambulio hilo la Sinjar lilikuwa moja ya sababu zilizoifanya Marekani kuanza mashambulizi ya angani kusambaratisha ngome za IS nchini Iraq, baada ya kuibuka kwa wasiwasi wa kutekelezwa kwa mauaji ya halaiki.

Marekani baadaye ilipanua mashambulio yake hadi Syria mwezi uliofuata.