Kundi la IS lakiri kutekeleza shambulizi Paris

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa islamic state

Kundi la kigaidi la Islamic State limekiri kutekeleza shambulizi la Paris.

Katika taarifa yake iliochapishwa mtandaoni,kundi hilo la kijihadi ,limesema kuwa shambulizi hilo lililenga kuielezea Ufaransa kwamba pia nayo ni miongoni mwa mataifa yanayolengwa na kundi hilo.

Kundi hilo limesema kuwa lilichunguza maeneo yalioshambuliwa na kutekeleza mashambulizi hayo kwa kuwatumia ndugu wanane waliovalia mikanda ya vilipuzi mbali na kujihami na bunduki.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Paris

Tangazo hilo lilitolewa katika maandishi ya kifaransa na kiarabu na kwa sauti zote kupitia idhaa za wapiganaji wa IS kulingana na mtaalamu BBC wa habari za wanajihad Peter King.

Taarifa hiyo inadai kwamba ndugu wanne waliovalia vilipuzi na kujihami na bunduki waliyalenga maeneo yaliotengwa katikati mwa mji wa Ufaransa.

Taarifa hiyo pia imeendelea na kutaja mji wa Paris kama mji mkuu wa 'uchafu na upotoshaji'.

Image caption Ujumbe wa IS

''Katika shambulizi takatifu ,kundi la waumini la Ukhalifa -mwenyezi mungu alipe nguvu na ushindi-lililenga mji mkuu wa uchafu na upotoshaji,mji unaobeba bendera ya msalaba barani Ulaya,Paris''.