Wanafunzi wa chuo waandamana DR Congo

Mgomo
Image caption Vyumba vya wanafunzi vinadaiwa kuporwa

Wanafunzi wa chuo kikuu kimoja nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo leo wameandamana Kinshasa kulalamikia kuongezwa kwa ada ya masomo.

Wanafunzi hao kutoka taasisi ya taifa ya uhandisi wamefunga barabara na kuchoma magari matatu karibu na bewa la chuo kikuu hicho.

Mwandishi wa BBC Poly Muzalia anasema baadhi ya vyumba vya wanafunzi pia vimeporwa.

Image caption Magari matatu yameteketezwa chuoni

Polisi wamewakamata waandamanaji 10, anaripoti.

Ada ya masomo imeongezeka kutoka takriban $300 (£200) hadi $500.