Maafisa 1,900 wa usalama kuajiriwa Uingereza

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa zaidi wa usalama kuajiriwa Uingereza

Uingereza imeongeza bajeti kwa vitengo vyake vya usalama nchini humo baada IS kutangaza kuhusika na mashambulio hayo ya Paris .

Waziri mkuu David Cameron amesema fedha hizo zataboresha idara za kintelligensia kama vile MI5, MI6 na GCHQ na kuongeza maafisa 1900.

Cameron ameonya kuwa mashambulio kama yaliyofanyika nchini Ufaransa yanaweza kufanyika Uingerzea.

Hata hivyo akasema atafanya kazi pamoja na washirika wake ikiwa ni pamoja na serikali za mataifa ya bara Ulaya ilikusaidiana kupambana dhidi ya Islamic State.

Aidha Cameron amesisitiza kuwa Britain itaimarisha ulinzi wa mipaka yake kufuati mauaji hayo mjini Paris.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Waziri mkuu David Cameron amesema fedha hizo zataboresha idara za kintelligensia kama vile MI5, MI6 na GCHQ na kuongeza maafisa 1900.

Cameron amekiri kuwa kupigana dhidi ya dhana hiyo potovu sio jambo rahisi na kuwa ni'' tatizo la enzi ya leo''.

Mawaziri wanatarajiwa kuidhinisha nyongeza ya mgao wa fedha kwa ajili ya tishio hilo la ugaidi.

Habari hii ilitolewa mapema kulikoilivyopangwa kufuatia hofu iliyozuka baada ya kuibuka kwa shambulizi la Paris.