Lori 100 za mafuta zashambuliwa Syria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lori 100 za mafuta zashambuliwa Syria

Muungano wa majeshi unoongozwa na Marekani ulishambulia wanamgambo wa Islamic State.

Muungano huo umeharibu zaidi ya malori 100 mashariki mwa Syria katika eneo ambalo wanamgambo wa Islamic State huendesha shughuli zao.

Msemaji wa Pentagon amesema ni mara ya kwanza majeshi hayo kufanikiwa kushambulia idadi kubwa ya malori ya mafuta kwa wakati mmoja.

Magari hayo yalikuwa yameegeshwa katika eneo moja.

Image caption Muungano wa majeshi unoongozwa na Marekani ulishambulia wanamgambo wa Islamic State.

Wanamgambo wa IS hupata mamilioni ya dola kila mwezi kutokana na mauzo ya mafuta katika ngome yao.

Majeshi hayo ya muungano yanajaribu kusambaratisha uwezo wa kifedha wa kundi hilo.

Hayo yanaripotiwa wakati ndege za kivita za Ufaransa zikifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi huko Syria mjini Raqqa, dhidi ya wanamgambo wa IS.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za kivita za Ufaransa zikifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi huko Syria mjini Raqqa, dhidi ya wanamgambo wa IS

Harakati hizo za mashambulizi zimeimarishwa siku mbili baada ya kundi hilo kutangaza kwamba ndilo lilihusika na mashambulio yaliyosababisha vifo vya watu 129 huko Paris.

Is wamesema walifanya mashambulio hayo baada ya Ufaransa kujiunga na vikosi vya muungano ambao umekuwa ukishambulia kundi hilo.

Wizara ya ulinzi ya Ufaransa imesema harakati zao huko Syria zimelenga maeneo ya silaha , na maeneo yanayotumiwa na kundi hilo kwa mafunzo na mazoezi .