Operesheni ya Urusi yaongeza wakimbizi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Urusi Vladmir Putin

Operesheni ya jeshi la Urusi nchini Syria inaongeza idadi ya wakimbizi wanaosafiri kwenda Ulaya, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk ameeleza.

Akiongea kwenye mkutano wa G20 nchini Uturuki, Bw Tusk ameihimiza Urusi iwalenge wapiganaji wa Islamic State na si dhidi ya upinzani nchini humo.

Urusi imekuwa ikitekeleza mashambulizi ya anga ikidai kulenga IS.

Lakini wengi wanahofu kuwa nia ya Urusi ni kuendelea kumuweka mshirika wake, Rais wa Syria, Bashar Al Assad madarakani.

Mkutano wa G20 wa viongozi wa dunia ulilenga maswala ya uchumi, lakini mkutano huo wa siku mbili ulitawaliwa na tukio la mashambulizi ya Paris.