Nigeria yakumbwa na mzozo wa mafuta

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa Nigeria Muhammadu

Misururu mirefu imeonekana kwenye vituo vya uuzaji mafuta nchini Nigeria,kutokana na sababu ya kuwepo mgawanyiko baina ya serikali na waagizaji mafuta kutokana na kutolipwa kwa ruzuku.

Serikali ya Nigeria tayari ilikwisha idhinisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni mbili kama malipo ya malimbikizo ya nyuma,lakini Rais Muhammadu Buhari amesisitiza kuwa suala hilo liwasilishwe bungeni.

Utawala ulioondoka madarakani nchini humo ulilipa ruzuku bila ya kuwashirikisha wabunge,lakini rais Buhari ameahidi kupambana narushwa.

Inadaiwa kuwa waagizaji hao wa mafuta wanadai kwamba madai yao ya ruzuku ya mafuta ni ndogo ukilinganisha na faida wanayoipata.

Pamoja na kwamba ni wazalishaji wakubwa wa mafuta,Nigeria inalazimika kuagiza mafuta nje ya nchi hiyo karibu lita milioni arobaini za petroli kwa matumizi ya kila siku ya madereva wake,huku ikiwa na viwanda vitatu tu vya kusafisha mafuta ghafi.