Nina virusi vya Ukimwi, akiri Charlie Sheen

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Muigizaji nguli wa Hollywood, Charlie Sheen amejitokeza wazi na kufichua kuwa anaugua virusi vya ukimwi.

Muigizaji nguli wa Hollywood, Charlie Sheen amejitokeza wazi na kufichua kuwa anaugua virusi vya ukimwi.

Sheen aliyepata umaarufu zaidi kwa kuigiza katika filamu ya ''Two and a half men'', alifichua hali yake katika mahojiano na runinga ya Marekani.

‘’Niko hapa kukiri mimi nina virusi’’ ‘’Ni maneno machungu’’ alisema.

Sheen amesema hafahamu alikotoa ugonjwa huo ila analaumu unywaji wa pombe na madawa ya kulevya kwa hali yake.

Muigizaji huyo ameongeza kusema kuwa anaendelea kutumia madawa ya kupunguza makali ya ukimwi na amekuwa akifuata maagizo kwa umakini.

Sheen alimsimulia mtangazaji wa NBC, Matt Lauer kuwa alichoshwa kuwalipa watu pesa iliwafiche hali yake kutokana na unyanyapaa.

‘’nimelazimika kusimamisha madai na uchafuzi wa jina langu na ukweli usiojiri’’ aliongeza.

Sheen alifichua kuwa alipatikana na virusi hivyo yapata miaka minne iliyopita.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uaminifu wangu uligeuka kuwa mateso’’. Alisema Sheen.

Alikariri kuwa alipowafahamisha rafiki zake juu ya hali yake, alikumbwa na usumbufu mwingi ikiwemo vitisho na kuitishwa pesa.

‘’Nilikuwa naamini kuwa walikuwa wandani wangu, wangenisaidia.

Uaminifu wangu uligeuka kuwa mateso’’. Alisema Sheen.

Sheen aliongeza kuwa kahaba mmoja alichukua picha ya majibu ya ukaguzi wa afya yake na kutisha kusambaza kwa magazeti.

‘Nafikiri leo nimejifungua kutoka gereza hili,’’

Daktari Robert Huizenga aliyeandamana na Sheen, alieleza kuwa msanii huyo hana Ukimwi.

Haki miliki ya picha AP FX
Image caption Miongoni mwa filamu alizoigiza ni Platoon, Wall Street na mwaka wa 2011, alikuwa muigizaji aliyelipwa zaidi duniani.

Miongoni mwa filamu alizoigiza ni Platoon, Wall Street na mwaka wa 2011, alikuwa muigizaji aliyelipwa zaidi duniani.

Hata hivyo mabadiliko kwenye tabia zake zilimfanya abanduliwe kutoka filamu hiyo.

Baadaye alianza kufanyiwa ushauri juu ya matumizi ya dawa za kulevya.

Sheen ameoa mara tatu na kupata watoto nne wakiwemo wavulana wawili na wasichana wawili.

Ndoa yake na Scottine Ross iliyopangwa kufanyika pia imeahirishwa.