Almasi kubwa yapatikana Botswana

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Almasi

Jiwe la pili lenye thamani zaidi duniani la Almasi limegunduliwa nchini Botswana.

Jiwe hilo limepatikana katika mgodi wa Karowe Kaskazini mwa mji mkuu , Gaborone.

Ndiyo almasi kubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini Botswana na pia katika muda wa zaidi ya karne moja.

Almasi kubwa zaidi iliwahi kupatikana nchini Afrika Kusini mwaka elfu moja mia tisa na tano.

Botswana ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa Almasi duniani hali ambayo imeinua pato la uchumi la nchi hiyo.