Ongezeko la talaka lakumba mji wa Uturuki

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uturuki

Mji mmoja wa Uturuki uliokaribu na mpaka wa Syria umeshuhudia ongezeko la talaka katika muda wa mwaka mmoja.

Mawakili katika mji huo wa Sanliurfa wanasema idadi kubwa ya kesi za talaka ni kutokana na wanaume kuchumbia wakimbizi wa kike kutoka Syria.

Licha ya kuwa ni kinyume cha sheria kuoa zaidi ya mke mmoja nchini Uturuki, baadhi ya wanaume katika maeneo ya waarabu na Wakurdi hufuata utamaduni wa kuoa wake wengi.