Visa vipya vya Ebola vyatangazwa Liberia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ebola Liberia

Maafisa wa afya wa Umoja wa Mataifa wanasema kumetokea maambukizi mapya ya Ebola nchini Liberia chini ya miezi mitatu baada ya nchi hiyo kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo.

Mgonjwa wa sasa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kumi kutoka viungani mwa mji wa, Monrovia.

Wachambuzi wanasema habari hii ni pigo kubwa kwa nchi ya Liberia ambayo imeshuhudia zaidi ya maambukizi elfu kumi na vifo zaidi ya elfu nne tangu ugonjwa wa Ebola kugunduliwa nchini humo.