New Zealand kupigia kura bendera mpya

Bendera Haki miliki ya picha New Zealand Govt
Image caption Bendera hizo zinapeperushwa maeneo mengi kuwezesha raia kufanya uamuzi

Raia nchini New Zealand wawanapiga kura kuchagua bendera ambayo huenda ikachukua nafasi ya bendera ya sasa.

Kura hiyo ya maamuzi itapigwa kuanzia Novemba 20 hadi Desemba 11 kupitia posta kuamua bendera moja kati ya tano zilizopendekezwa ambayo ni bora zaidi.

Kutafanyika kura nyingine mwaka 2016 kuamua iwapo bendera mpya itakayochaguliwa kwenye kura ya kwanza inafaa kuchukua nafasi ya bendera ya sasa ambayo huwa na bendera ya Uingereza almaarufu Union Jack.

Waziri Mkuu John Key amesema bendera ya sasa haiakisi New Zealand ya sasa.

Image caption Michoro mingi ina picha ya kangaga

Aidha, anaamini inafanana sana na bendera ya Australia lakini amekiri kwamba ishara zinaonyesha huenda raia wengi wa New Zealand wakaamua kusalia nayo.

Image caption Kangaga ni nembo ya taifa la New Zealand

Michoro minne ya bendera iliorodheshwa kupigiwa kura Septemba lakini ikakosolewa kwa madai kwamba ilifanana sana au haikuwa na ubunifu.

Baada ya kampeni kali mitandao ya kijamii, bendera ya tano iliongezwa.

Image caption Bendera hii ni tofauti na nne za kwanza

Bendera hizo zimewekwa maeneo mengi kote nchini humo kwa raia kujionea na kufanya uamuzi.

Aidha, zinatolewa bure kwa watu na makundi ya kijamii yenye milingoti mitano ya kuzipeperushia.