Wakatoliki wanaongezeka sana Afrika

Kenya
Image caption Kenya ndilo litakuwa taifa la kwanza kuwa mwenyeji wa Papa Francis Afrika

Papa Francis yumo kwenye ziara yake ya kwanza Afrika ambayo itaendelea hadi Novemba 30.

Aliaanzia Kenya, na sasa yuko Uganda na anatarajiwa kumalizia Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wakatoliki wanaongezeka sana Afrika kuliko bara jingine lolote duniani na Mapapa wa awali walifanya ziara nyingi barani.

Ukatoliki Kenya, Uganda, C.A.R.

Kenya

  • Wakristo 82.5% (Waprotestanti 47.4%, Wakatoliki 23.3%, wengine 11.8%), Waislamu 11.1%, Watamaduni 1.6%, wengine 1.7%, wasio na dini 2.4%, wasioelezwa 0.7% (Chanzo: CIA World Factbook)
  • Wakatoliki: 8,970,000 (Chanzo:Pew Research Center)

Uganda

  • Wakatoliki 41.9%, Waprotestanti 42% (Waangilikana 35.9%, Wapentekosti 4.6%, Waadventisti (SDA) 1.5%), Waislamu 12.1%, wengine 3.1%, wasio na dini 0.9% (Chanzo: CIA world Factbook)
  • Wakatoliki: 14,100,000 (Chanzo: Pew Research Center)

C.A.R.

  • Watamaduni 35%, Waprotestanti 25%, Wakatoliki 25%, Waislamu 15% (Chanzo: CIA World Factbook)
  • Wakatoliki: 1,260,000 (Chanzo: Pew Research Center)

Nchini nyingine zenye Wakatoliki wengi

  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo: 31,180,000 (wengi zaidi Afrika)
  • Nigeria: 20,040,000
  • Tanzania: 14,250,000
  • Angola: 10,850,000