Ubelgiji yaonya kuhusu Shambulio

Haki miliki ya picha Sbastien GEORIS RTBF
Image caption Ubelgiji.usalama waimarishwa kufurtai onyo la shambulio

Ubelgiji imeimarisha hali yake ya tahadhari katika eneo la mji mkuu wa Brussels, ikionya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mashambulizi.

Safari za reli na magari ya kusafiri chini ya ardhi - vyote vimesimamishwa hadi kesho.

Raia wameonywa wasitembelee maeneo yenye mikusanyiko kama vile vituo vya biashara na vile vya michezo.

Hali ya tahadhari katika maeneo mengine ya nchi iko chini kidogo lakini bado kuna hali ya wasiwasi.

Ubelgiji haswa Brussels pamekuwa mahali ambapo washukiwa wengi wa mashambulizi ya Paris ya Ijumaa iliyopita wanadhaniwa kuishi.

Mmoja wa wale wanaotafutwa ni Salah Abdeslam, anayedhniwa anaishi Ubelgiji sasa kwa maficho