Van Gaal:Mchezo wa Depay umeshuka

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa anatarajia mengi kutoka kwa winga wa klabu hiyo Memphis Depay.

Depay mwenye umri wa miaka 21, aliigharimu United kitita cha pauni milioni 31 wakati alipojiunga na klabu hiyo kutoka PSV Eindhoven msimu huu lakini hajaanzishwa tangu klabu hiyo iliposhindwa na Arsenal 3-1 mnamo mwezi Octoba.

Van Gaal alisema:Tunatarajia mengi kutoka kwa kwake ndio hachezeshwi.''lakini wachezaji katika umri huo huwa sio thabiti,sijakosana na mchezaji huyo,ni kwamba mchezo wake umeshuka tu''.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Memphis Depay

Depay alifunga mabao 22 wakati PSV Eindhoven iliposhinda taji lake la kwanza la ligi tangu mwaka 2007-2008 msimu ulioipita.

Alifunga mara moja tu katika ligi ya Uingereza tangu alipojunga na timu hiyo,na hajachezeshwa katika mechi nne zilizopita,huku Jesse Lingard akipewa kipao mbele.