Muungano wa mataifa ya Asia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Muungano wa mataifa ya Asia

Viongozi wa nchi kumi za muungano wa kusini mashariki mwa Asia zimetia sahihi makubaliano ya kubuni jamii ya kiuchumi ya ASEAN.

Hatua hiyo ilichukuliwa kwenye mkutano uliofanyika mjini Kuala Lumpur nchini Malaysia na inaupeleka hatua moja mbele muungano wa ASEAN kuwa eneo la biashara huru kwa watu millioni 600,000.

Bado vizuizi vimesalia laikini waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak anasema kwa muungano huo tayari umeondoa vizuizi vya kodi.