Tope la sumu lakaribia ufukweni Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Tope la sumu lakaribia ufukweni Brazil

Tope la taka ya sumu linalosafirishwa na mto Rio Doce nchini Brazil linatarajiwa kuwasili kwenye ufukwe wa bahari ya Atlantic saa chache zinazokuja.

Haki miliki ya picha Associacao dos Pescadores e Amigos do Rio Doce
Image caption Tope hilo lina sumu inayotokana na madini ya chuma

Tope hilo la sumu ya chuma lilitokea baada ya bwawa lililoko karibu na timbo la madini ya chuma kuvunja kingo zake majuma mawili yaliyopita.

Inakisiwa kuwa tope hilo limesafirishwa zaidi ya kilomita 500 kutoka eneo la milimani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Udongo huo umesombwa umbali wa kilomita 500 tangu bwawa hilo kuvunjika zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Kampuni inayomiliki mgodi huo (- Samarco -) imekuwa ikijenga vizuizi katika mto Rio Doce ikijaribu kuwakinga wanyama na mimea kutoka kwa udongo huo wenye taka nyingi ya chuma.

Udongo huo umesombwa umbali wa kilomita 500 tangu bwawa hilo kuvunjika zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Eneo ambapo mto huo unaingilia bahari ni mazingira muhimu kwa samaki na kasa

Eneo ambapo mto huo unaingilia bahari ni mazingira muhimu kwa samaki na kasa mbali na viumbe wengine walio kwenye hatari ya kuangamia.

Wafanyikazi wa kampuni hiyo wamekuwa wakiwashika kasa waliokuwa wanataga mayai na kuwahamisha katika maeneo salama kabla ya udongo huo kuwasili.