Hofu ya ugaidi imeiwacha Brussels mahame

Haki miliki ya picha AP
Image caption Brussels ni mahame

Mikahawa na maeneo ya burudani kati kati ya mji wa Brussels nchini Ubelgiji yamebakia mahame baada ya utawala kuamri maeneo yote ya umma kufungwa mapema kutokana na tishio la mashambulizi.

Mwandishi wa BBC katika mji huo anasema kuwa mitaa ilibakia mahame huku polisi na wanajeshi wakionekana wakipiga doria na kuendesha misako katika maeneo yanayoshukiwa uwa maficho ya wahusika wa shambulizi la kigaidi lililotokea Ufaransa majuzi.

Mikutano ya hadhara pamoja na mikusanyiko yote ilipigwa marufuku.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Vyombo vya dola vinafuata vidokezi muhimu kwa nia ya kumkamata japo wanasema kuwa wamegundua washirika wengi mno wa njama kama hiyo.

Inaanimika kuwa mmoja wa washukiwa wakuu wa njama ya kuishambulia Paris Salah Abdeslam alitorokea Ubelgiji baada ya kufanya mashambulizi hayo.

Sasa vyombo vya dola vinafuata vidokezi muhimu kwa nia ya kumkamata japo wanasema kuwa wamegundua washirika wengi mno wa njama kama hiyo.

''Tunajua hata tukimkamata Salah Abdeslam tishio la ugaidi halitatoweka kwani sasa tumegundua kuwa kunahatari kubwa zaidi ya watu ambao wanaweza kutekeleza mashambulizi'' alisema waziri wa usalama wa ndani bwana Jan Jambon.

Waziri mkuu Charles Michel alisema kuwa kumekuwa na habari za uwezekano wa kutokea shambulizi sawa na lililotokea mjini Paris wiki iliyopita.

Serikali ya Ubelgiji huenda ikatoa tahadhari ya usalama baadaye leo Jumapili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Treni za chini kwa chini zimesitisha safari zake mjini Brussels

Rafiki zake Abdeslam, wameaimbia runinga moja ya Marekani kuwa wamezungumza naye kwa njia ya Skype na akawambia kuwa yuko Brussels akitafuta njia za kurejea Syria.

Yamkini anashukiwa kuwa amejihami kwa ukanda wa vilipuzi.

Aidha serikali ya Marekani imewaonya raia wake wasiondoke majumbani mwao kwa hofu ya kutokea mashambulizi ya kigaidi.