Mzozo kuhusu mshindi wa 'Mr Ugly' Zimbabwe

Haki miliki ya picha
Image caption Mison Sere, alitajwa kuwa mshindi wa tuzo la mwaka huu la mtu mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe.

Nchini Zimbabwe kumefanyika mashindano ya kipekee ya kumpigia kura mwanaume mwenye sura mbaya zaidi katika taifa hilo.

Kama mashindo mengine ya urembo shindano hili pia lilivutia washiriki wengi.

Jopo la majaji lilikua na mengi ya kutahini kando na sura walitizama hulka na kujitanua kwa washindani

Lakini walipotoa uamuzi wao vurugu lilitibuka kisa na maana .....

Kihoja kilizuka pale waamuzi walipomtaja Mison Sere, kuwa mshindi wa tuzo la mwaka huu la mtu mwenye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe.

Image caption Sere na mkewe walishangilia ushindi wao mkubwa

Hata hivyo mashabiki wa bingwa mtetezi,William Masvinu walilalamikia uamuzi huo wakidai kuwa bwana huyo alikuwa na sura nzuri tu licha ya mwanya mkubwa na tabasamu kama ya kibogoyo.

Licha ya majibizano makali Sere mwenye umri wa miaka 42 alituzwa mshindi na kutuzwa dola mia tano ($500).

Yeye na mke wake walishangilia tuzo hilo jukwaani na kuwatonesha kidonda wafuasi wa mpinzani wake waliowazomea na hata kuzua vurugu wakidai kapendelewa.

'Walihoji umauzi wa majaji wakisema kuwa hakuwa na sura mbaya ila alikuwa ka'ngoa meno yake ya mbele.'

''hayo sio maumbile ya kutisha kukosa meno?

Image caption William Masvinu alilalamikia uamuzi huo wakidai kuwa bwana huyo alikuwa na sura nzuri tu !

''Inakuwaje wanampuuza bingwa wa zamani William Masvinuambaye maumbile yake yanatisha mno''

Mwisho wa mjadala huo ulibakia vivyo hivyo.

Bingwa mara tatu wa tuzo la mtu mwnye sura mbaya zaidi nchini Zimbabwe William Masvinu alikwenda nyumbani katika nafasi ya pili.

'Huyu bwana hatishi kamwe,hebu tizama pua langu kubwa uso wangu mwusi na unavyotisha,sikio langu ni kama la popo ni kubwa itakuwaje kuwa amenishinda ?'

'La sikubaliani na uamuzi huu wa leo, nimeudhika sana.'' Masvinu alisikika akinungunika.