Unaweza kuigiza sokwe? Kuna kazi

Dawn Haki miliki ya picha TWENTIETH CENTURY FOX
Image caption Filamu ya Dawn of The Planet of The Apes ilitolewa mwaka 2014

Je, ungependa kujiunga na mwigizaji mashuhuri Andy Serkis katika kuigiza filamu mpya ya msururu wa filamu za Planet of the Apes? Hapa kuna nafasi.

Waandalizi wa filamu hizo 20th Century Fox wameanzisha shindano kwa watu ambao wangelipenda kushiriki katika filamu filamu ijayo ambayo imepewa jina War for the Planet of the Apes.

Filamu hiyo imepangiwa kuzinduliwa 2017.

Unachohitajika kufanya ni kujipiga video ukiwa unaigiza sokwe mtu na kisha uitume kwa waandalizi wa filamu hiyo katika apescontest.com.

Serkis amekuwa akiigiza kama Caesar, mwazilishi wa himaya ya sokwe na ataendelea kuigiza nafasi hiyo. Waigizaji wapya watakuwa Woody Harrelson na Steve Zahn.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waigizaji wa Dawn of The Planet of The Apes

Filamu hiyo itakuwa ya tatu kwenye msururu wa filamu hizo, ya kwanza ikiwa Rise of the Planet of the Apes na ya pili Dawn of the Planet of the Apes ambayo ilitolewa mwaka uliopita.