'Platini akabiliwa na marufuku ya kudumu'

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Michel Platini

Makamu wa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Michel Platini huenda akapigwa marufuku ya kudumu asishiriki katika maswala yote ya soka kulinagana na mawakili wake.

Afisa huyo wa UEFA kwa sasa anahudumia marufuku ya siku 90 kufuatia madai ya ufisadi pamoja na rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter,huku kamati ya FIFA ikiangazia hatua itakayochukua.

Wakili wa Platini Thibaud d'Ales amesema kuwa ripoti ya wachunguzi hao wa maadili ni kashfa kubwa.

Kamati hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wake mwezi ujao.

Image caption Blatter na Platini

Raia huyo wa Ufaransa anakabiliwa na vikwazo kuhusu malipo yasiotakiwa ambayo yalimwezesha Platini kupata pauni milioni 1.35 kutoka kwa Blatter mwaka 2011 kwa kazi ya ushauri iliofanywa miaka tisa iliokwisha.

Wawili hao ambao wanahudumia marufuku ya siku tisini wamekana kufanya makosa yoyote lakini wakakiri kwamba hakuna makubaliano yalioandikwa chini.