Uturuki 'yadungua ndege ya Urusi Syria'

Ndege Haki miliki ya picha Anadolu
Image caption Runinga ya taifa imeonyesha ukanda wa video ulioonyesha ndege ikianguka

Ndege za kijeshi za Uturuki zimeripotiwa kudungua ndege ya kijeshi ya Urusi karibu na mpaka wake na Syria.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema ndege aina ya Su-24 ilianguka katika ardhi ya Syria baada ya ksuahmbuliwa kutoka ardhini, na kwamba marubani walifanikiwa kutoka kabla ya ndege hiyo kushika moto na kuanguka.

Lakini maafisa wa jeshi la Uturuki wanasema ndege za kijeshi za Uturuki aina ya F-16 zilishambulia ndege hiyo baada ya kuionya kwamba ilikuwa imeingia anga ya Uturuki bila idhini.

Runinga ya taifa ya Uturuki imepeperusha ukanda wa video unaoonyesha ndege ikianguka milimani karibu na mpaka wake na mkoa wa Latakia.

Inaaminika ndege hiyo imeanguka katika eneo linalodhibitiwa na waasi.

Ndege za kijeshi za Syria na urusi zimekuwa zikishambulia wapiganaji wa Kiislamu pamoja na waasi wanaoungwa mkono na mataifa ya Magharibi eneo hilo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za kijeshi aina ya Su-24 zimekuwa zikitumiwa na Urusi kushambulia wapinzani wa Rais Bashar al-Assad