Uganda: Bunge lazindua kituo cha kunyonyesha

Image caption Bunge la Uganda limezinduaa kituo cha kuwanyonyesha watoto.

Bunge la Uganda limezinduaa kituo kipya ambapo wabunge pamoja na watumishi wa bunge watakuwa wanakitumia kuwanyonyesha watoto.

Hiki ndicho kituo cha kwanza nchini Uganda kuweka kituo kama hicho katika nafasi za kazi.

Mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango anatuaarifu zaidi.

Image caption Uganda: Bunge lazindua kituo cha kunyonyesha

Watoto wanapiga makelele wakicheza ndani ya kituo walichoita cha kuwanyonyoshea watoto ambapo kuna vifaa mbalimbali vya kuwafurahisha watoto hata na wale ambao ni wachanga lakini hawanyonyeshi.

Miongoni mwa vitu vya kuchezea kama vile puto za rangi tofauti lakini pia kuna televisheni ambako kuna video za katuni.

Kituo hiki ni cha manufaa kwa wanaoendesha kazi zao mahali hapo, wabunge pamoja na watumishi.

Josephine Watera, mfanyakazi bungeni, anasema kuwa alikabiliwa na wakati mgumu alipohitajika kuja ofisini wakati wa likizo yake akiwa mjamzito.

Lakini kwa kuwa kituo hiki kimefunguliwa sasa anaweza kuendelea na kazi zake bila bughudha akijua kuwa mtoto wake atakuwa karibu naye.

Image caption Kituo hiki ni cha manufaa kwa wanaoendesha kazi zao mahali hapo, wabunge pamoja na watumishi.

''nikiwa hapa naye ninajua kuwa amepata kitu cha kula ikilinganishwa na hali ya kutegemea jibu la simu yaani unampigia simu mtu nyumbani kumuuliza ikiwa mtoto ameshakula -jibu litakuwa ndio hata ikiwa hajala.''

''Lakini hapa nitajua kuwa mtoto amepata maziwa na nikirejea katika mmeza yangu nitakuwa mtulivu kabisa.''

Spika wa bunge la Uganda Rebecca Kadaga, amesema kuwa taasisi hiyo inaweka mfano wa kuigwa na taasisi zote za serikali na hata za kibinafsi nchini humo.

''Naomba wafanya kazi watumie vilivyo kituo hiki ili kusiwe na kisingizio hiki wala kile.''

''Unakumbuka enzi hizo wakati baadhi ya wafanyakazi wakija na watoto wachanga na kuwaacha kwenye maegesho siku mzima? anauliza bi Kadaga.

Image caption Yaya wa Uganda hawana ujuzi mwingi.

''Na tungeshtakaiwa kwa kupuuza haki za watoto wa Uganda kwa kubaki ndani ya jua siku nzima.'' anasema bi Kadaga.

Yaya wa Uganda hawana ujuzi mwingi.

Uelewa wa wengi kuhusika na utoaji wa huduma hiyo au kumshughulikia mtoto mchanga kama vile wa miezi miwili ni finyu mno

likizo ndefu kwa mama mjawazito inayotolewa na kampuni nyingi ni karibu siku 90.