Ghasia:Watu 75 waachiliwa huru Burundi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ghasia zilizokuwa nchini Burundi.Takriban watu 75 waliohusika katika ghasia hizo sasa wameachiliwa huru

Mahakama nchini Burundi imetangaza kuachiliwa huru kwa watu 75 kati ya zaidi ya watu 250 waliozuiliwa kuhusiana na ghasia zinazoendelea nchini humo.

Wengine wamepokea vifungo vifupi zaidi ya ilivyoagizwa na mwendesha mashataka.

Maandamano ya ghasia yalianza mnamo mwezi Aprili wakati rais Nkurunziza alipotangaza kuwa atasimama kwa awamu ya tatu.

Kumekuwa na mauaji mengi ambayo hayaeleweki nchini humo tangu kuchaguliwa tena kwa Nkurunziza,huku serikali ikipokea shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa kusitisha vitendo zaidi vya ukandamizaji.