Phuc Dat Bich akiri kufanya mzaha kuhusu jina lake

Haki miliki ya picha Phuc Dat Bich
Image caption Phuc Dat Bich

Raia mmoja wa taifa la Australia anayejiita Phuc Dat Bich ,ambaye aligonga vichwa vya habari duniani baada ya kusema kwamba alikuwa akitaka kutumia jina lake sahihi katika mtandao wa facebook amekiri kwamba ilikuwa mzaha.

Bwana Bich amesema katika mtandao wake wa facebook kwamba jina lake rasmi ni Joe Carr{ ama Joker}.

Amesema kuwa kile alichoanzisha kati ya marafiki ulikuwa mzaha mkubwa katika vyombo vya habari.

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Phuc Dat Bich

Mtu huyo ni raia wa Vietnam.Jina lake linapotamkwa vizuri kwa lugha ya Vietnam husikika kama ''Phoo Da Bi''.

Facebook haijatoa tamko lolote kwa BBC kuhusu maoni yake.