Mwanamke wa Iran apata agizo la jaji kushiriki katika soka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Soka ya wanawake

Mwanamke mmoja ambaye ni nyota wa soka nchini Iran amefanikiwa kushiriki katika mchuano mmoja ughaibuni baada ya jaji kuzuia juhudi za mumewe za kumtaka kutosafiri.

Mwanamke aliyeolewa nchini Iran anahitaji ruhusa ya mumewe kuondoka nchini humo.

Niloufar Ardalam aligonga vichwa vya habari wakati mumewe alipomzuia kutosafiri ili kushiriki katika mashindano nchini Malaysia mnamo mwezi Septemba.

Lakini Ardalan ambaye ni nahodha wa kikosi cha taifa hilo amesema kuwa alifanikiwa kupata agizo la jaji kusafiri,na amefanikiwa kushiriki katika mchuano unaoendelea nchini Guatemala.