Mancity kuchuana na Juve bila wachezaji 6

Haki miliki ya picha PA
Image caption Pellegrini

Klabu ya Manchester City itacheza bila wachezaji wake sita muhimu itakapokutana na Juventus.

City ambao wamefuzu katika makundi ya timu 16,itamkosa beki Eliaquim Mangala,Pablo Zabaleta na Vincent Kompany,viungo wa kati Samir Nasri,David Silva na mshambuliaji Wilfried Bony.

''Tuna hali ngumu'', alisema meneja Manuel Pellegrini.''Ni mtihani wa kushinda katika uwanja wa timu ngumu''.

City inaiongoza Juventus kwa pointi moja kileleni mwa kundi Da na itathibitisha uwezo wake kama mshindi wa kundi hilo.

Image caption wachezaji wa Mancity

''Kila mtu ameikosoa klabu hii kuhusu mchezo wake barani Ulaya'',alisema Pellegrini kuhusu City,ambayo haijafuzu katika makundi ya timu 16 katika vilabu bingwa Ulaya.

Kwa hivyo ni muhimu kwetu kupata mafanikio miongoni mwao ikiwa kufuzu katika makundi ya timu 16.