Urusi yakatiza Uhusiano na Uturuki

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waziri mkuu wa Urusi , Dmitriy Medvedev, amesema kuwa Uturuki inawalinda Islamic State

Urusi imeonya kuwa italipiza kisasi kufuatia kuangushwa kwa ndege yake.

Waziri mkuu wa Urusi , Dmitriy Medvedev, amesema kuwa Uturuki inawalinda Islamic State .

Medvedev amedai kuwa Uturuki inahofia kupoteza kipato kikubwa inachofaidika kutokana na wizi wa mafuta kutoka Syria.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Urusi inadai Uturuki inafaidika na wizi wa mafuta kutoka kwa Islamic state

Aidha, Medvedev amedai kuwa mikataba yote na Uturuki imesimamishwa na kuwa kampuni zote zenye asili ya Uturuki zimepigwa marufuku nchini Urusi.

Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.

Hakikisho hilo la rais Obama linafwatia hatua ya Uturuki kuidungua ndege ya Urusi karibu na mpaka wa Syria.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Obama amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.

Mataifa yote duniani yalihofia kutibuka kwa vita iwapo Moscow ingelipiza kisasi kufuatia mauaji ya askari wake katika shambulizi hilo.

Ikulu ya WhiteHouse ilisema kuwa wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya marais hao wawili kuwa wote walikubaliana kutuliza hali hiyo.

Umoja wa mataifa na muungano wa kujihami ya nchi za Maghraibu NATO wamewataka Urusi na Uturuki kutuliza hasira zao.

Akizungumza baada ya mkutano wa dharura wa mataifa ya NATO ulioitishwa na Uturuki, katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema tathmini ya tukio hilo inaonyesha kuwa ndege ya kivita ya Urusi iliruka katika anga ya Uturuki.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waasi wanaungwa mkono na Uturuki wakiwa na mabaki ya mwavuli uliotumika na marubani wa Urusi

Huku kukiwa na hali ya wasiwasi, Stoltenberge ametaka kuwepo na hali ya utulivu kutoka pande zote.

Amesema taarifa walizozipokea kutoka nchi washirika, zinaenda sambamba na maelezo ya Uturuki ya tukio hilo.

"Ushirikiano tulioupata kutoka kwa washirika mbalimbali kwa leo unathibitisha taarifa tuliyoipata kutoka Uturuki."

Hata hivyo, Moscow bado wanasisitiza kwamba, ndege hiyo ilikuwa katika anga ya Syria, na kwamba hakukuwa na ukiukwaji wa anga ya Uturuki.