Ugonjwa wa akili waathiri uchumi Australia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri Mkuu wa Australia

Magonjwa ya akili huathiri sana uchumi wa Australia na hivyobasi huduma zinahitaji kuangaziwa upya kulingana na waziri mkuu Malcolm Turnbull.

Bwana Turbul amezindua mbinu mpya ambayo amesema itatoa huduma bora kwa wagonjwa.

Mpango huo utaruhusu utumiaji zaidi wa teknolojia.

Australia hutumia dola bilioni 10 kila mwaka kwa huduma za magonjwa ya akili.

Ugonjwa wa aakili unaathiri uzalishaji wa taifa na kushiriki kwa raia katika maswala ya kujenga taifa.

Mkakati huo mpya ambao utazinduliwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2016,unajiri baada ya serikali kuangazia upya mfumo wa afya ya akili wa Australia.

Huduma kama vile za simu za dharura zitaimarishwa huku vituo vya matibabu vikiruhusiwa kuweka mipango yake ya kuwahudumia wagonjwa walio na mahitaji tata.