Mkutano kukomesha ndoa za utotoni

Haki miliki ya picha seetu tiwari
Image caption Binti mdogo aliyeolewa

Umoja wa Afrika leo unaanza mkutano wa siku mbili utakaofanyika Zambia kukomesha ndoa za utotoni barani.

Inakadiriwa kwamba mwanamke mmoja kati ya watatu barani Afrika ameolewa kwa ruhusa ya wazazi, walezi na viongozi wa kidini katika umri wa miaka 18. Idadi hiyo inatarajia kuongezeka ifikapo mwaka 2050.

Mamia ya wasichana wa kike waliokuwa na ndoto za kuenda shule wamejikuta wakilazimika kuwa mama, baada ya kulazimisha kuolewa mapema.

Nyingi ya ndoa hizo za mapema hufanyika vijijini, ambako utamaduni bado unanguvu.

Umoja wa Afrika na mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali yameunganisha nguvu kushawishi serikali mbalimbali kufanya ndoa za utotoni kama jambo lisilo halali kisheria, kutokana na kukinza haki ya mtoto kupata elimu na pia kumuathiri afya yake.