Kiongozi Muislamu amsifu Papa, Kenya

Image caption Hassan Omar

Seneta muislamu nchini Kenya ametoa maoni yake kuhusu ziara ya papa Francis nchini Kenya kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa kiongozi wa kanisa katoliki duniani.

Akizungumza na chombo cha habari cha AP Seneta huyo Hassan Omar amesema kuwa Papa Francis hajabagua dini yoyote.

''Amezungumza kuhusu hali ya raia wa Palestina,walio dhaifu na walionyanyaswa.Ni mnyenyekevu na ameonyesha wazi kwamba ni mtetezi wa haki za jamii '',alisema Omar Hassan.