Trump: Amkejeli mwandishi habari mlemavu

Haki miliki ya picha APTN
Image caption Trump akimuigiza mwandishi mlemavu wa New York Times

Mmoja wa wagombea kiti cha chama cha Republican Donald Trump amezomewa baada ya kumkejeli mwandishi wa habari mlemavu wa jarida la New York Times

Trump alijikunyata akiigiza anavyokaa mwandishi huyo Serge Kovaleski.

Yamkini alimnukuu ripota huyo ambaye mwaka wa 2001 aliandika habari iliyodai kuwa maelfu ya waislamu walishangilia magaidi walipodungua ndege za abiria katika shambulizi la septemba tarehe 11.

Jarida la New York Times limekashifu sana hatua ya Trump wakiitaja kuwa jambo la ''kushtua''

Bwenyenye huyo alinukuu ripoti hiyo ya mwandishi Kovaleski ya mwaka 2001 na kudai kuwa ''ni ripota mzuri sana''

Trump alikuwa akihutubia mhadhara wa wafuasi wake katika mji wa South Carolina jumanne usiku.

Haki miliki ya picha twitter
Image caption Trump alikwenda kwenye mtandao wake wa Tweeter na kuiponda jarida la New York Times

Sasa maskini huyu bwana , lazima umuone huyu mwandishi wa habari, kisha akaguna na kuweka mikono yake akiigiza anavyokaa bwana Kovaleski,

"Uhh siamini nilichokisema .Labda sikusema,labada nilisema hivyo.''

Bwana Kovaleski anaugua '''arthrogryposis'' ugonjwa unaolemaza uwezo wa viungo vyake kutembea na inaonekana sana katika upande wake wa kulia haswa mkono.

Msemaji wa New York Times samenukuliwa akisema ''ni jambo la kustaajabisha na kuhuzunisha sana kuwa anakejeli mwandishi wetu''