Pombe kupigwa marufuku Bihar, India

Haki miliki ya picha Sanjay Kumar
Image caption Nitish Kumar

Waziri mkuu wa jimbo la Bihar nchini India ,Nitish Kumar ametangaza mipango ya kupiga marufuku uuzaji na utumizi wa pombe katika jimbo hilo.

Bwana Kumar awali alikuwa amewaahidi wapiga kura kwamba atazuia ufunguaji wa maduka ya kuuza pombe katika vijiji.

Hatua hiyo italigharimu jimbo la Bihar zaidi ya dola milioni 500 za kodi,kulingana na msemaji wa chama tawala cha Bihar Janata Dal.

Pombe imepigwa marufuku katika majimbo kadhaa ya India ikiwemo Gujarat na Manipur.

Bwana Kumar anaongoza muungano wa vyama vya kijimbo vilivyochukua mamlaka katika jimbo la Bihar mapema mwezi huu.

Wakati wa kampeni zake,alikabiliwa na maandamano ya wanawake ambao walilalama kuhusu ubugiaji mbaya wa pombe katika vijiji.

Image caption Nitish Kumar

''Nahisi kwamba wanawake wanapata shinda zaidi ya wengine kutokana na unywaji wa pombe....nimeagiza maafisa wangu kuanza harakati za kupiga marufuku na kuanza kuidhinisha hatua hiyo kuanzia kipindi kijacho cha fedha,bwana Kumar alisema katika mkutano mwengine siku ya Alhamisi.

Mwaka uliopita,serikali kusini mwa Kerala ilitangaza mipango ya kuzuia uuzaji na unywaji wa pombe kwa mika 10.

Wamiliki wa baa na wale wa hoteli wamelipinga agizo hilo kwenye mahakama huku marufuku hiyo ikipunguzwa ili kuruhusu baa kuuza pombe na mivinyo.