Wapalestina 2 wauawa,wanajeshi 4 wajeruhiwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Palestina

Wapalestina 2 wameuawa baada ya mashambulizi ya magari ambapo wanajeshi 4 Waisraeli walijeruhiwa.

Katika shambulio moja, Mpalestina mmoja aliendesha gari lake akiwaelekeza wanajeshi wawili wa Israel katika kituo cha mabas karibu na Ufuo wa Magharibi katika mji wa Kfar Adumim.

Wanajeshi hao walijeruhiwa kidogo.Mpalestina huyo alipigwa risasi na kuuawa papo hapo.

Mshambuliaji huyo alitambuliwa kama Hasib Fadi, mwenye umri wa miaka 30, mkaazi wa Ramallah.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ghasia kati ya Palestina na Israel

Shambulio sawa na hilo lilifanywa katika mji wa Wapalestina wa Beit Umar, Kusini mwa Jerusalem, ambapo wanajeshi sita walijeruhiwa.

Mshambuliaji alitambuliwa kama Issa Arafat, mwenye umri wa miaka 18.

Yeye pia alipigwa risasi na kujeruhiwa.