Madrassa kudhibitiwa Uingereza

Image caption Mwanafunzi katika Madrassa

Shule za Madrassa nchini Uingereza zinakabiliwa na udhibiti na ukaguzi chini ya mipango ya serikali iliochapishwa siku ya Alhamisi.

Mwezi uliopita waziri Mkuu David Cameron alisema kuwa baadhi ya watoto walikuwa 'wakipewa sumu na kufunzwa chuki' katika madrassa.

Mashirika ya kiislamu yanakubali kwamba udhibiti unahiitajika ili kuwalinda watoto lakini yananisistiza kuwa wasiwasi kuhusu msimamo mkali haufai.

Uingereza ina takriban madrassa 2,000.