Uturuki yamuonya Putin ''kutocheza na moto''

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Erdogan wa Uturuki na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin katika mkutano wa siku za hapo nyuma.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuonya mwenzake wa Urusi Vladimir Putin 'kutocheza na moto' kuhusu swala la taifa lake kuidungua ndege ya kijeshi ya Urusi.

Bwana Erdogan pia amesema kuwa anataka kukutana na bwana Putin ana kwa ana katika mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa ili kusuluhisha mzozo huo.

Bwana Putin anataka kuombwa msamaha na Uturuki kabla ya kuzungumza na Erdogan ,msaidizi wa rais huyo amesema.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ndege ya Urusi iliodunguliwa na Uturuki

Urusi imeamua kusitisha mpango wa kusafiri bila viza miongoni mwa raia wa mataifa hayo mawili kwa mujibu wa waziri wa maswala ya kigeni nchini humo.

Uturuki inasema kuwa ndege hiyo ilikuwa katika anga yake ilipolengwa,lakini Urusi inasema kuwa ilikuwa katika anga ya Syria.

''Ningependa kukutana na bwana Putin ana kwa ana mjini Paris'',alisema bwana Erdogan katika hotuba yake katika runinga.

''Ningependa kusuluhisha tatizo hili.Inaudhi kuona kwamba swala hili limeongezewa chumvi''.

Haki miliki ya picha
Image caption Mgogoro kati ya Urusi na uturuki kufuatia kuduguliwa kwa ndege ya Urusi na Uturuki

Lakini pia amesema kuwa Uturuki haitaki kuharibu uhusiano wake na Urusi.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov ameonya kuwa kisa hicho kinaweza kuathiri maslahi ya Uturuki.