Maafisa 4 wa usalama wauawa Misri

Image caption Saqqara Misri

Maafisa wanne wa usalama nchini Misri wameuawa katika shambulio la uendeshaji kulingana na maafisa wa usalama.

Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Saqqara kilomita 35 kusini mwa mji mkuu wa Cairo.

Washambliaji wasiojulikana walikuwa wakiendesha pikipiki wakati walipowafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kizuizi kimoja cha barabarani kulingana na ripoti za chombo cha habari cha Reuters.

Misri imekumbwa na mashambulio yanayowalenga maafisa wake wa usalama tangu jeshi limuondoe aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi mnamo mwezi Julai Mwaka 2013.