Je,wadudu wanafaa kuwa chakula cha nguruwe na kuku

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Nguruwe

Wanasayansi wa Ulaya wameanzisha utafiti rasmi kuamua iwapo kuwalisha ngurue na kuku wadudu ni salama kwa afya zao na walaji.

Kulingana na utafiti unaoungwa mkono na shirika la Ulaya la Usalama wa Chakula, funza waliokaushwa au nzi wa kawaida wa nyumbani wanakaushwa na kusagwa kabla ya kuchanganywa na nafaka inayotumiwa kulisha ngurue na kuku.

Matumizi ya protini katika utengenezaji wa vyakula vya mifugo yamepigwa marufuku tangu kuzuka kwa maradhi ya kichaa cha ng'ombe miaka ya 80.

Hatua hii imeleta upungufu mkubwa wa protini katika chakula cha mifugo.

Image caption Chicken

Inaaminika kuwa wadudu wana kiwango cha juu zaidi cha protini hadi asilimia 60.

Mradi huo unataka kuthibitisha iwapo mifugo hao wanaweza kula vyakula vilivyochanganywa na wadudu hao kwa njia ambayo watanufaika bila kusababisha maafa kwa watumizi wa bidhaa ya mifugo au kuku hao.

Wanasayansi wanasema kuwa iwapo mpango huo utafaulu, chakula hicho kinaweza kuwa mbadala wa maharagwe ya soya.