Uchina kumaliza ufukara 2020

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Uchina

Shirika la habari la taifa la Uchina, linasema kuwa viongozi wanamaliza mkutano wa siku mbili kuhusu namna ya kuondosha umaskini, ifikiapo mwaka wa 2020.

Uchumi wa Uchina umekuwa haraka katika miongo mitatu iliyopita, na kuwatoa mamilioni ya watu kwenye umaskini, yaani pato la chini ya dola moja kwa siku.

Lakini watu zaidi ya milioni 70 wa mashambani, bado ni maskini.

Baadhi ya sera za kumaliza umaskini, ni kujenga miji haraka, na kutoa mikopo kwa wakulima wawe wajasiria mali.

Wachambuzi wanasema, kupunguza tofauti kubwa baina ya matajiri na maskini inaonekana kuwa njia ya kuendeleza utulivu.