Fury amchapa Klitschko na kutwaa ubingwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bondia Muingereza,Tyson Fury ndiye bingwa wa dunia wa uzani mzito.

Bondia Muingereza,Tyson Fury ndiye bingwa wa dunia wa uzani mzito.

Bondia huyo Muingereza,Fury alimtamausha mshikilizi wa taji la uzani wa mzito duniani Wladimir Klitschko na kutwaa ukanda wa dunia.

Tyson alimpiku raia huyo wa UKraine Klitschko kwa wingi wa pointi katika pigano hilo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Fury, aliibuka mshindi wa jumla ya pointi baada ya marefarii wote watatu kumpa pointi nyingi zaidi ya Klitschko.

Ushindi huo wa Fury ulikatiza ubabe wa Klitschko wa miaka 9 akiwa ni bondia bingwa wa uzani wa juu.

Fury, aliibuka mshindi wa jumla ya pointi baada ya marefarii wote watatu kumpa pointi nyingi zaidi ya Klitschko.

Muingereza huyo alizoa alama 115-112, 115-112, 116-111 na hivyo kutawazwa bingwa wa dunia wa uzani wa juu wa taji la WBA, IBF na WBO.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Muingereza huyo alizoa alama 115-112, 115-112, 116-111

Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 27- ameingia katika orodha ya mabingwa wa dunia wa uzani wa juu wa ndondi baada ya Bob Fitzsimmons, Lennox Lewis, Frank Bruno na David Haye.

Muingereza huyo ambaye aliwasili katika mahojiano na waandishi wa habari akiwa amevalia mavazi ya ''Batman'' aliwapa mashabiki wake elfu 50,000 walifika katika ukumbi wa Esprit Arena, sababu ya kutabasamu baada ya kumtandika Klitschko makonde mazito mazito huku akikwepa na kujitanua ulingoni.