Urusi imeiwekea Uturuki vikwazo vya kiuchumi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Urusi imeiwekea uturuki vikwazo vya kiuchumi

Urusi imetangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Uturuki kutokana na kudunguliwa kwa ndege yake mnamo Jumanne.

Rais wa Urusi Vladmir Putin ametia sahihi amri ambayo inapiga marufuku kununuliwa kwa bidhaa kutoka Uturuki, kuzuia shughuli za viwanda fulani vya Uturuki vilivyoko Urusi.

Raia wa Uturuki pia hawataajiriwa kazi nchini Urusi.

Amri hiyo pia inapiga marufuku safari za ndege zilizokodishwa kibinafsi kati ya mataifa hayo mawili.

Image caption Raia wa Uturuki pia hawataajiriwa kazi nchini Urusi.

Amri hiyo itaanza kutekelezwa tarehe mosi mwezi Januari mwakani.

Awali Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan alieleza masikitiko yake kufuatia kudunguliwa kwa ndege hiyo lakini akakosa kuomba msamahaka.