Brazil:Homa ya Zika husababisha ulemavu wa watoto

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Homa ya Zika husababishwa na mbu mwenye asili ya Afrika

Wizara ya Afya ya Brazil imetangaza rasmi kuwa kuna uhusiano kati ya homa kali ya Zika inayosambazwa na mbu kutoka Afrika na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa nchini humo na ulemavu.

Wizara ilisema kuwa homa hiyo ijulikanayo kama Zica, iliyotangazwa kwa mara ya kwanza kuwa nchini humo Aprili mwaka huu, inahusika na kuwepo kwa matukio mengi ya maradhi ya 'micro-encephalitis' - ambayo husababisha uvimbe wa ubongo wa mtoto tumboni miezi mitatu kabla ya kuzaliwa .

Homa hii husababisha kichwa cha mtoto aliye tumboni kuwa kidogo.

Haki miliki ya picha Edmar Melo JC Imagem
Image caption Brazil imetangaza kuwa kuna uhusiano kati ya homa kali inayosambazwa na mbu kutoka Afrika na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na ulemavu nchini humo .

Wizara ya afya ya Brazil imesema kuwa imegundua matukio 730 ya maradhi hayo Ceara iliyoko Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo.

Watu wawili pia wamefariki kutoka na homa ya Zica, juma hili.

Wizara imesema kuwa hii ni mara ya kwanza kwa homa hiyo aina ya Zica kusababisha kifo na maumivu kabla ya mtoto kuzaliwa.

Madkatari bingwa kutoka shirika la afya duniani, WHO, na Marekani wanatarajiwa Brazil baadaye juma hili.